Miguel Gamondi Atangaza Kikosi cha Awali cha Taifa Stars kwa AFCON 2025

Kocha wa Taifa Stars, Miguel Gamondi, ametangaza leo Desemba 3, 2025, kikosi cha awali cha wachezaji 53 kitakachoshiriki maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Kikosi hiki, kinachojumuisha wachezaji wanaoshughulika kwenye ligi za ndani na nje ya Tanzania, kitaratibiwa kuondoka nchini Disemba 8, 2025, kuelekea Nchi ya Misri, kwaajili ya kambi ya maandalizi kabla ya mashindano.

Gamondi amesema kuwa hatua hii ya awali ni muhimu kwa kutambua wachezaji wenye fomu bora, kuunganisha timu na kuweka mikakati kabla ya AFCON. Kikosi kitapitia mazoezi makali, mechi za kirafiki, na tathmini ya kina ya kila mchezaji, ili kisha kupunguzwa hadi idadi rasmi ya wachezaji 23 itakayoshiriki mashindano.

Taifa Stars inatarajia kuanza mashindano ya AFCON wakiwa na lengo la kufanikisha historia nzuri, huku wakijivunia wachezaji wenye uwezo wa kimataifa na wa ndani.