Yanga SC vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC ni vinara wa ligi msimu wa 2025/26 ambao una ushindani mkubwa.

Ushindi kwenye mchezo dhidi ya KMC FC uliochezwa Novemba 9,2025 unawapa tiketi ya kuwa namba moja kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 4.

Awali ni watani zao wa jadi walikuwa hapo baada ya Mbeya City kujenga utawala wao katika nafasi hiyo kwa muda.

Yanga SC imefikisha jumla ya pointi 10 ikiwa imecheza mechi 4 za ligi. Simba SC ni nafasi ya pili ikiwa na pointi 9 baada ya kucheza mechi 3.

Pamba Jiji ni nafasi ya tatu pointi 9 baada ya mechi 6 huku Mbeya City ikiwa nafasi ya 4 na pointi zake ni 8 baada ya mechi 6.

Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari Yanga SC amesema kuwa ni muhimu kujivunia timu hiyo kutokana na ubora walionao na matokeo ambayo yanapatikana uwanjani.

“Ni muhimu kujivunia timu yetu ya Yanga SC ambayo inaongoza ligi ni timu namba moja kufunga mabao mengi na imefungwa mabao machache,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.