Erling Haaland ameendelea kuonesha ubora wake ndani ya Ligi Kuu ya England baada ya kufunga bao lake la 14 msimu huu, akiipatia Manchester City uongozi dhidi ya Liverpool kwenye mchezo unaopigwa katika uwanja wa Etihad Stadium.
Bao hilo la kwanza lilifungwa dakika ya 29, kabla ya Nico kuongeza la pili katika dakika ya 45+4, na kufanya vinara hao wa EPL kwenda mapumzikoni wakiwa vifua mbele kwa mabao 2-0.
City wameonekana kutawala mchezo kwa asilimia kubwa ya umiliki wa mpira, huku Liverpool wakionekana kushindwa kupata nafasi za wazi mbele ya safu imara ya ulinzi ya wenyeji.
⏸ HT: Manchester City 2-0 Liverpool
⚽ 29’ Erling Haaland
⚽ 45+4’ Nico