Simba SC vs Nsingizini Hotspurs, msafara ndani ya Eswatini kazi kuanza

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs, msafara umewasili salama ndani ya Eswatini kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya mwisho kuelekea katika mchezo huo wa kimataifa.

Wawakilishi hao wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika kete ya kwanza watakuwa ugenini na ile ya pili itamalizwa Dar katika Uwanja wa Mkapa.

Ikumbukwe kwamba Oktoba 16 usiku kikosi hicho chini ya Menaja Mkuu Dimitar Pantev kiliwasili Eswatini wakitokea Afrika Kusini.

Mchezo ujao kwa Simba SC ni ugenini dhidi ya Nsingizini Hotspurs unatarajiwa kuchezwa Oktoba 19 2025 ikiwa ni raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya mchezo huo ule wa marudiano itakuwa ni Simba SC vs Nsingizini Hotspurs, Oktoba 24,2025, CAF Champions League, Uwanja wa Mkapa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.