WIKIENDI itakuwa bize kutokana na kazi kubwa kwa wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa kusaka ushindi kwenye mechi ambazo watashuka uwanjani.
Hapa tunakuletea ratiba za mechi hizo na muda utakaochezwa kwa saa za Afrika Mashariki namna hii:-
Ligi ya Mabingwa Afrika
Jumamosi, Yanga SC watakuwa Uwanja wa Bingu nchini Malawi dhidi ya Silver Striker, kuwania kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mechi hii itachezwa kuanzia saa 10:00 jioni na kuruka mbashara kupitia AzamSports2HD.
Jumapili, Simba SC watakuwa Eswatini katika Uwanja wa Somhlolo wakicheza na Nsingizini Hotspurs kuwania kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mechi hii itachezwa kuanzia saa 10:00 jioni na kuruka mbashara kupitia AzamSports2HD.
Kombe la Shirikisho Afrika
Jumamosi, KMKM watakuwa Uwanja wa Amaan wakiwakaribisha matajiri wa Chamazi, Azam FC.
Mechi hii itachezwa kuanzia saa 10:15 jioni na kuruka mbashara kupitia AzamSports4HD.
Jumapili, Singida BS watakuwa jijini Bunjumbura katika Uwanja wa Prince Louis Rwagasore wakicheza na Flambeau Du Centre.
Mechi hii itachezwa kuanzia saa 10:00 jioni, na kuruka mbashara kupitia AzamSports4HD.
***
Na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.