Simba SC kuwafuata wapinzani wao kimataifa Eswatini

WAWAKILISHI wa Tanzania katika anga la kimataifa Simba SC wanatarajiwa kukwea pipa kesho Oktoba 16 kuelekea Eswatini kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba SC ina kibarua cha kusaka ushindi raundi ya kwanza ya CAF Champions League dhidi ya Nsingizini Hotspurs kikiwa ugenini.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 19,2025 na ule wa marudinao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 24,2025.

Katika kete ya pili Uwanja wa Mkapa itatoa maamuzi ya mwisho ya nani ambaye atatinga hatua ya makundi kwenye anga la kimataifa.

Msafara unatarajiwa kuwa na watu 50, wachezaji 22, benchi la ufundi lenye watu 12 pamoja na viongozi wengine wa timu hiyo.

Huo utakuwa ni mchezo wa kwanza wa ushindani kwa Meneja Mkuu wa Simba SC, Dimitar Pantev mrithi wa mikoba ya Fadlu Davids ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Raja Casablanca.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.