YANGA SC WAPO KAZINI, KUMSHUSHA WINGA WA KAZI

KLABU ya Yanga ipo katika mazungumzo ya mwishoni katika kuipata saini ya winga wa Singida Black Stars, Edmund John ili awe sehemu ya kikosi hicho katika msimu ujao.

Inadaiwa makubaliano binafsi kati ya mchezaji na Yanga tayari yamekamilika na mchezaji yupo tayari. Nyota huyo alikuwa tishio katika mchezo wa Nusu Fainali wa Kombe la CRDB dhidi ya Simba.

Yanga wamempatia mkataba wa miaka mitatu winga huyo, kilichobakia makubaliano kati ya Yanga na Singida Black Stars yapo hatua za mwishoni kukamilika ili nyota huyo asaini.

Tayari Yanga SC ipo kambini kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26 wakiwa kwenye mazoezi ya awali kuelekea msimu mpya.

Yanga SC ni mabingwa watetezi kwa msimu ujao baada ya kutwaa taji msimu wa 2024/25 wakiwa na pointi 82 baada ya mechi 30.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.