BAADA ya kucheza mechi 28 ambazo ni dakika 2,520 safu ya ushambuliaji ya Yanga SC imefunga mabao 76 na kukusanya pointi 76 ikiwa namba moja kwenye msimamo na timu iliyofunga mabao mengi.
Kwenye mchezo wake wa raundi ya 29 dhidi ya Tanzania Prisons, Yanga SC ilikomba pointi tatu mazima kwa ushindi wa jumla ya mabao 0-5 iliposepa na pointi tatu ugenini, Uwanja wa Sokoine, Mbeya ilikuwa Juni 18 2025.
Yanga SC kwenye mchezo huo bao la tano lilifungwa na Pacome dakika ya 75 akiwa ni mchezaji aliyefunga mabao mawili kwenye mchezo huo na alichaguliwa kuwa mchezaji bora.
Ni mabao 11 anafikisha ndani ya ligi Pacome akiwa kiungo aliyehusika kwenye jumla ya mabao 20 kati ya 76 yaliyofungwa na timu hiyo kwa kuwa ametengeneza jumla ya pasi 9 za mabao kwenye mechi za ligi.
Timu ambayo imefungwa mabao mengi kwenye ligi ni KenGold ambayo ni 57. Baada ya kucheza mechi 29 ambazo ni dakika 2,610 safu ya ushambuliaji ya KenGold imefunga jumla ya mabao 22 ikikusanya pointi 16 msimu wa 2024/25.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.