VITA YA UFUNGAJI BORA PASUA KICHWA

Kwenye eneo la tuzo ya kiatu cha ufungaji bora vita bado ni mbichi kutokana na mechi ambazo zimebaki matokeo yake kutotabirika.

Jean Ahoua wa Simba SC ni kinara kwa sasa akiwa na mabao 16 anafuatiwa na Clement Mzize na Prince Dube wa Yanga SC wakiwa wametupia mabao 13. Leonel Ateba wa Simba SC naye katupia mabao 13.

Kupata maumivu kwa Prince Dube kunapunguza mwendo kidogo kwa washambuliaji wa Yanga SC anabaki Mzize pekee katika vita hiyo huku Pacome akiwa katika ubora wake na mabao yake 11.

Ili Ahoua atwae tuzo ya ufungaji bora ni lazima afunge katika mechi zijazo kwa kuwa kila mchezaji amekuwa katika vita yake.

Jonathan Sowah wa Singida Black Stars ni ingizo jipya dirisha dogo ila ameonyesha ubora kwenye kucheka na nyavu, mabao 12 ni mchezo mmoja umebaki kwa Singida Black Stars itakuwa dhidi ya Tanzania Prisons Juni 22 2025.

Yanga SC vs Simba SC ni mechi mbili zimebaki kwao ambazo ni dakika 180 zitakazoamua vita ya kiatu cha ufungaji bora msimu wa 2024/25.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.