ELVIS RUPIA KWENYE RADA ZA YANGA SC

Mkali kwenye kucheka na nyavu ambaye yupo Singida Black Stars, Elvis Rupia anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Jangwani Yanga SC ambao wanahitaji saini yake kwa ajili ya msimu mpya wa 2025/26.

Rupia ndani ya ligi katupia mabao 10 akiwa namba mbili kwenye eneo hilo ndani ya Singida Black Stars na kinara ni Jonathan Sowah mwenye mabao 11.

Singida Black Stars inatarajiwa kucheza fainali ya CRDB Federation Cup dhidi ya Yanga SC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Juni 28 2025.