Mamelodi Sundowns wamekuwa washindi wa pili mbele ya Pyramids FC ambao ni mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Pyramids FC ya Misri ni mabingwa wapya Afrika ikipata ushindi mbele ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini kwenye fainali ya pili.
Kwenye fainali nyota Fiston Mayele mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Juni Mosi wakati wakishinda mabao 2-1 Mamelodi Sundowns, Mayele kwenye mchezo huo alitupia bao moja.
Pyramids FC walifunga bao la kusawazisha katika dakika za mwisho za mchezo wa kwanza na kupata sare muhimu. Bao hilo liliwapa matumaini na kupunguza presha kuelekea mchezo wa nyumbani na kuwapa ari ya kubadili matokeo.
Costa ndiye aliyefunga bao pekee la Sundowns kwenye mchezo wa kwanza. Kiungo huyo kutoka Brazil mwenye umri wa miaka 26 alijaribu kurudia kiwango chake bora Juni Mosi lakini alishindwa safu ya kiungo na timu yake kuipa ubingwa timu hiyo.
Kwenye fainali ya pili iliyopigwa Cairo, Misri Uwanja: 30 June Air Defence VAR ilitumika na mwisho bingwa amepatikana ambaye ni mwarabu kutoka Misri.
Ikumbukwe kwamba hata kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Simba SC wamekuwa washindi wa pili mbele ya RS Berkane ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika. Hivyo mataji yote makubwa Afrika 2024/25 yamebebwa na Waarabu.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.