BAADA ya kupoteza kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika wa hatua ya robo fainali ya kwanza, Uwanja wa Suez Canal, Misri, shabiki wa Simba maarufu kwa jina la Kinyago wa Simba wa Tabata amebainisha kuwa wanaamini mchezo wao ujao dhidi ya Al Masry, Uwanja wa Mkapa watafanya kweli na kutinga hatua ya nusu fainali.
Aprili 4 alfajiri wachezaji wa Simba ikiwa ni Elie Mpanzu, Jean Ahoua, Shomari Kapombe, Ladack Chasambi wamerejea Dar kwa maandalizi ya mchezo ujao unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.