SIMBA WAKISHINDA DHIDI YA BRAVOS ITAKUWA HIVI

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wakipata matokeo dhidi ya Bravos watakuwa wamejihakikisha nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Tayari kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kipo nchini Angola kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo wao dhidi ya Bravos amba oni wa hatua ya makundi unatarajiwa kuchezwa Januari 12 2025.

Ally amesema kuwa kwa namna ambavyo kundi lipo kila mchezo ni mgumu kwa kuwa pointi zao tisa walizonazo haziwapi nafasi kutinga hatua ya robo fainali hivyo watapambana kupata matokeo ugenini.

“Ni pointi tatu muhimu kwetu ambazo tunazihitaji tukiwa ugenini, benchi la ufundi na wachezaji wanatambua kwamba tukipata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu dhidi ya Bravos tutakuwa tumefanikisha malengo ya kufuzu hivyo hesabu itabaki mchezo mmoja ambao tutakuwa nyumbani.

“Kila kitu kinakwenda saw ana ushindani ni mkubwa hivyo mashabiki wazidi kutuombea dua tunaamini kwamba tutafanya vizuri na kupata matokeo chanya kwenye mchezo wetu mgumu ndani ya uwanja.”

Miongoni mwa wachezaji waliopo Angola ni Jean Ahoua, Mavambo, Kibu Dennis, Camara, Ally Salim.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.