MWALIMU AWEKWA KWENYE RADA ZA TIMU KUBWA BONGO

MSHAMBULIAJI namba moja kwa utupiaji ndani ya Fountain Gate ni Suleman Mwalimu ambaye katupia mabao 6 msimu wa 2024/25. Taarifa zinaeleza kuwa Mwalimu amewekwa kwenye hesabu za timu kubwa Bongo ambazo zipo ndani ya tatu bora.

Ikumbukwe kwamba mbali na kuwa namba moja kwa Fountain Gate ni namba moja kwa wazawa wenye mabao mengi kinara kiujumla ni nyota Elvis Rupia kutoka Kenya.

Fountain Gate baada ya kucheza mechi 14 imekusanya pointi 20 ikiwa nafasi ya 6 kwenye msimamo na safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 23.

Taarifa zinaeleza kuwa vinara wa Ligi Kuu Bara, Azam FC hawapo mbali kufuatilia saini ya nyota huyo huku Yanga na Simba nao wakitajwa kuwa kwenye hesabu za kuinasa saini ya nyota huyo.

Yanga tayari wameshamalizana na baadhi ya nyota kinachosubiriwa ni kutambulishwa na mchezaji wa kwanza kutambulishwa ni Israel Mwenda ambaye yupo hapo kwa mkopo akitokea Singida Black Stars.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.