ADEMOLA LOOKMAN ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA SHIRIKISHO LA SOKA AFRIKA (BALLON D’OR)

Mshambuliaji wa klabu ya Atalanta ya Italia na timu ya taifa ya Nigeria, Ademola Lookman ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Shirikisho la soka Afrika (Ballon d’or) kwenye tuzo za CAF zilizofanyika Mjini Marrakesh , Morocco.

Lookman (27) amewashinda Simon Adingra wa Ivory Coast, Serhou Guirassy wa Guinea, Achraf Hakimi wa Morocco na Ronwen Williams wa Afrika Kusini.