MR BLUE NI KABISA MKALI

UKIZUNGUMZIA Bongo Fleva kuna majina mengi yanapita yamefanya mapinduzi makubwa ikiwa ni pamoja na Sugu ambaye huyu ni muziki wa Hip Hop kiujumla alileta mageuzi makubwa ukiigusa ile ngoma ya Miaka 18 anasema ilikuwa ni stori ya kweli akaituma kwa jamii kupitia nyimbo.

Legend Dully Sykes huyu alileta mtindo wa Mwanasesere kisha Bongo Fleva ikaanza kuboresha kupitia yeye na ndio maana kweye ngoma yake ya Bongo Fleva alisema kuwa Bongo Fleva anaiweza, kuimba na kucheza.

Weka kando hawa utakumbuka ufalme wa Ferooz na starehe zama za Daz Nundaz yupo mkali wa michano huru wa muda wote na hajapatikana zaidi yake ambaye ni Ngwea…

Tupo na katili kwenye nyimbo za watu hata ngoma zake ni kazikazi zinakimbiza tangu zama za mapozi, pesa, Mboga Saba, Mbwa Koko anaitwa Mr Blue wengi hupenda kumuita Byser.

Sema asili ya Byser inatajwa kuwa ilitokana na mwamba kukimbiza kwenye kila kolabo alizokuwa anapewa na hata nyimbo zake mwenyewe alikuwa anazikimbiza mpaka watu wanamuogopa.

Hapo likaaibuka neno Kabisa kutokana na swaga za mjini akaitwa Byser Byblon Bizi yaani yupo bize kuwakimbiza wengine kwenye nyimbo alimtuliza PNC kwenye mbona akamtoa kijana akawa juu, kisha stori zinasema walizinguana hawa wana.

Nyakati fulani alikuwa anafananishwa na kushindanishwa na Joseline wa Niite Basi hapo Dully akawaunganisha pamoja kwenye ngoma ya Dhahabu, hiyo ilikuwa ni ya Taifa ilitikisa kila kona na mkali alijulikana ni nani alimkibiza mwingine.

Weka hilo kando unaikumbuka ile ngoma ya Tabasamu? Yule aliyekaa kwenye kiitikio wakati huo hakuwa na jina kubwa lakini kupitia ngoma hiyo akawa mkubwa na kazi zake zikaanza kuuliziwa Dunia nzima sio Tanzania tu.

Aliachia tupo Pamoja, unaamibiwa kuna sehemu aliimba uhalisia kwa kuwachana waliokuwa wanampa tabu maskani kisa kuwa bize na kitu cha Moshi huko.

Kibao kipi kinaishi kwako kwa mwamba huyu ambaye bado hajachuja na uwezo wake ni uleule…

Muziki unaishi na kazi nzuri zinadumu daima…

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.