#BREAKING: DK NDUGULILE AFARIKI DUNIA AKIPATIWA MATIBABU INDIA…

Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika na Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile amefariki dunia.

Dkt. Ndugulile amekutwa na mauti wakati akipatiwa matibabu nchini India.

Ameandika Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X akiambatanisha na picha ya Dkt. Ndugulile, “I hate death” kwa fasiri isiyo rasmi “Nachukia kifo”.

Taarifa iliyotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemnukuu Spika, Dkt. Tulia Ackson akisema:

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile. Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi”.