🔴#BREAKING: KARIAKOO -GHOROFA LILILOANGUKA NA KUUA WATU TAZAMA KINACHOENDELEA MUDA HUU

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema zoezi la uokoaji kufuatia ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika eneo la Soko la Kimataifa la Kariakoo linaendelea tangu kutokea kwa ajali hiyo na halikusitishwa kama baadhi ya taarifa zilivyoenea mitandaoni.

Akizungumza akiwa Kariakoo Chalamila amesema kuna watu bado wapo chinii, hivyo waokoaji wanaendelea na zoezi la uokoaji kwa kutoa huduma ya Oksijeni na maji na kwamba zoezi hilo linaendelea kutokana na mawasiliano ya baadhi ya watu ambao wapo chini ya ghorofa hilo.