Mwanamuziki Mkongwe Boniface Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kikii’ amefariki dunia.
Mwanamuziki huyo ambaye ameugua kwa muda mrefu, amefariki usiku wa kuamkia leo Novemba 15 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa akipatiwa matibabu
King Kikii atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika muziki wa dansi Tanzania. Kwa miaka mingi ameburudisha, amefundisha na kuelimisha jamii kupitia nyimbo zake
Enzi za uhai wake, King Kikiii alitamba na vibao mbalimbali kikiwemo cha ‘Kitambaa cheupe’.
Pumzika kwa amani Mzee wa Kitambaa Cheupe King Kikii.