MISS WORLD AFRICA 2024 ATEULIWA KUWA WAZIRI WA VIJANA BOTSWANA

Mlimbwende aliyenyakua taji nchini Botswana mwaka wa 2022, ambaye pia ni Miss World Africa 2024, Lesego Chombo ameteuliwa kuwa Waziri wa Vijana na Masuala ya Wanawake wa nchi hiyo.

Chombo, mwenye umri wa miaka 26, aliteuliwa na Rais Duma Boko.

Mrembo huyo ni mmoja wa Mawaziri sita waliozinduliwa chini ya Serikali mpya ya Rais Boko, huku Mawaziri kumi na wawili wengine bado hawajatajwa.

Makamu wa Rais Ndaba Gaolathe ameteuliwa kuwa Waziri mpya wa Fedha wa nchi hiyo.Stephen Modise, Daktari ambaye aliendelea na Masomo yake nje ya nchi, ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya wa Botswana.

Naibu waziri wa Afya wa Botswana ni Lawrence Ookeditse, ambaye pia ni Mbunge wa Nata-Gweta.