YANGA YAIPIGA MKWARA AZAM FC

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hawana hofu na wapinzani wao Azam FC licha ya timu hiyo kupata muda mrefu wa kufanya maandalizi kuelekea mchezo wao wa Dar Derby katika NBC Premier League.

Ikumbukwe kwamba Azam FC mchezo wake uliopita ilicheza dhidi ya Ken Gold na kupata ushindi wa mabao 4-1 inakutana na Yanga iliyotoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

Gamondi amesema kuwa hawakuwa na muda mrefu wa kufanya maandalizi kwa kuwa wametoka kucheza mechi mbili mfululizo tofauti na wapinzani wao Azam FC.

“Hakuna muda wa maandalizi kwa sasa unaona tumetoka kucheza mchezo wetu dhidi ya Singida Black Stars na nyuma pia tulitoka kucheza mchezo mwingine dhidi ya Coastal Union.

“Ambacho kimetokea kipo hivyo wachezaji wanapambana kufanya vizuri tofauti na wapinzani wetu ambao walikuwa na muda kwa ajili ya maandalizi kuelekea mchezo wetu ambao ni muhimu. Licha ya yote hayo bado tuna kikosi imara na wachezaji wazuri tuna amini kwamba tutapata matokeo mazuri.”

Yanga ni namba moja kwenye msimamo ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 8 inakutana na Azam FC yenye pointi 18 baada ya kucheza mechi 9 ikiwa nafasi ya 4 msimu wa 2024/25.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.