BAADA ya kupoteza kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa London ukisoma West Ham 2-1 Manchester United, Gary Neville ameweka wazi kuwa anafikiria Eric ten Hag atafukuzwa ndani ya timu hiyo.
Manchester Legend, Gary Neville amesema kuwa anaamini bosi wa Manchester United, Eric ten Hag ataondolewa katika majukumu yake ndani ya Manchester United, inayotumia Uwanja wa Old Traford kwa mechi za nyumbani.
Jumapili ya Oktoba 27 Manchester United walipoteza ugenini shukrani kwa bao la jioni la penalti iliyofungwa na Jarrod Bowen dakika ya 90 ambapo penalti hiyo ilibidi itazamwe kwenye VAR kutokana na utata kutokea baada ya tukio hilo ndani ya 18.
Bao pekee la Manchester United lilifungwa na Casemiro dakika ya 81 kabla ya Bowen kuvunjavunja mioyo ya United na bao la utangulizi kwa West Ham lilifungwa na Crysencio Summerville dakika ya 74.
Nyota huyo amesema:” Eric ten Hag anatafuta matatizo. Yupo nafasi ya 14 katika msimamo baada ya mechi 8 na mechi hizo ni kama asilimia 25 hivi ya msimu. Inakuwa ni mbaya kila wakati kutokana na ufanyaji kazi, United inapaswa kuwa juu lakini wamepoteza.”
Source: Mail Online Football.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.