NGOMA ilikuwa ngumu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, ubao wa Tanzanite Kwaraa Babati umesoma Fountain Gate 2-2 Mashujaa ikiwa ni come back ya kibabe jioni kabisa ambapo Fountain Gate waliwabana Mashujaa waliokuwa kwenye wakati mzuri kusepa na pointi tatu za ugenini.
Ni Mashujaa walitawala mchezo mwanzo mwisho ugenini na kupata bao la kuongoza dakika ya 15 kupitia kwa Seif Karihe na Hassan Ali dakika ya 28.
Nicholas Gyan alipachika bao dakika ya 34 kipindi cha kwanza na dakika 45 zikaisha ubao ukisoma Fountain Gate 1- 2 Mashujaa.
Dakika za lala salama wakati Mashujaa wakiwa na matumaini ya kusepa na pointi tatu, Salum Kihimbwa dakika ya 90+3 alipewa jukumu la kupiga faulo akaizamisha nyavuni.
Wakati akishangilia alionesha ule usela wa kizamani kwa kuonekana akiwatusi wachezaji wa Mashujaa kwa kidole jambo ambalo sio la kiungwana kabisa.