MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Simba, Jean Ahoua ni majanga kwa kuwa bado hayupo fiti baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, Oktoba 19 2024.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo dhidi ya Yanga Ahoua alichezewa faulo dakika ya 27, 36, 54, 78 na alicheza faulo dakika ya 12, 45 alionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Ramadhan Kayoko dakika ya 45.
Hakuwa kwenye kikosi kilichopata ushindi dhidi ya Tanzania Prisons, Oktoba 22 2024 ubao wa Uwanja wa Sokoine uliposoma Prisons 0-1 Simba kwa bao la Che Malone.
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu, Fadlu Davids amebainisha kuwa ripoti ya madaktari itaamua kama atakuwa kwenye kikosi kijacho ama la.
Ahoua ana pasi nne za mabao na kafunga mabao mawili ndani ya msimu wa 2024/25.
Baada ya kucheza mechi 7 ambazo ni dakika 630 wamekomba pointi 16 safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 13 huku Ahoua akiwa amehusika kwenye mabao sita ndani ya ligi.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.