CHAMA MZEE WA MAAMUZI MAGUMU

KIUNGO wa Yanga, Clatous Chama ni yuleyule wa maamuzi magumu kwenye mechi ambazo anapewa nafasi ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Oktoba 22 2024 alifunga bao lake la kwanza kwenye ligi kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18 mbele ya JKT Tanzania na alitoa pasi moja dakika ya 23 kwa Pacome ambaye alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo.
Kumbuka kwamba bao la Chama dakika ya 43 ni Pacome alisababisha faulo kwa kipa Richard Dennis ambaye alijichanganya na kudaka mpira nje ya eneo lake la 18 akaonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi wa kati Arajiga.
Kumbuka kwamba kwenye Kariakoo Dabi, Chama faulo aliyopiga dakika ya 86 ilibadili usomaji wa ubao kwenye mchezo huo uliochezwa Oktoba 19 ambapo Chama aliingia dakika ya 84 akichukua nafasi ya Aziz Ki.

Mwamuzi Ramadhan Kayoko alipotoa faulo kwa Yanga, Chama alipewa jukumu la kupiga faulo hiyo na katika harakati za Moussa Camara kuokoa ilirejea ndani ya 18 ikakutana na Maxi Nzengeli ambaye alipiga krosi iliyozaa bao baada ya Kelvin Kijili kwenye harrakati za kuokoa kujifunga.

Ipo wazi kuwa hata alipokuwa Simba faulo yake ya dakika ya 90 kwenye mchezo dhidi ya Azam FC ilibadili usomaji wa ubao ikawa ni Simba 1-1 Azam FC.

Bao la Azam FC kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Februari 2 2024 lilifungwa na Prince Dube dakika ya 14 akitumia pasi ya Pascal ambapo naye kwa sasa Dube yupo ndani ya Yanga.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.