SALEH JEMBE AMSHUSHA VYEO CHAMA – ”HAKUNA FREE KICK KALI PALE – MPIRA ULIKUWA UNATOKA”…

Mchambuzi mkongwe wa soka nchini Saleh Jembe, amefunguka kupitia Global TV, ameonyeshwa kutopendezwa na maamuzi mabovu yaliyofanywa na mwamuzi Ramadhani Kayoko, katika mchezo kati ya Simba na Yanga jumamosi iliyopita, akikiri kuwa Kwa mwamuzi wa viwango vya FIFA kama Kayoko haipendezi kufanya Maamuzi kama aliyoyafanya.

Jembe amezungumza hayo alipokuwa akifanya mahojiano na Global TV, ambapo alieleza kuwa mwamuzi msaidizi pia alitakiwa kubeba lawama katika tukio ambalo nyota wa Yanga Chadrack Boka alimfanyia madhambi Kibu Denis, akidai mwamuzi msaidizi alikuwa jirani zaidi.

Aidha, Salehe Ally huyo aliongeza kuwa mchezo kama wa dabi ya Kariakoo hautakiwi kuwa na Lawama Kwa waamuzi, badala yake watu wazungumze kufungwa kutokana na uwezo wao au makosa yao na sio mwamuzi kubeba lawama zote.