KOCHA YANGA AANIKA SILAHA za MAANGAMIZI KUELEKEA DERBY ya KARIAKOO – ATAJA KIKOSI – VIDEO

Kauli ya kocha wa Yanga Sc Miguel Gamondi kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Simba Sc.

Tuna furaha kubwa kuelekea kwenye ligi huku tukiwa na mchezo muhimu wa Derby. Tupo vizuri, tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri hapo kesho. Hatujabadilika sana kwenye maandalizi tumejiandaa kama ambavyo tumekuwa tukifanya hapo awali”

“Tumetokea kwenye wiki ya FIFA na mara nyingi tunapata changamoto kidogo ya maandalizi kwani wachezaji wetu wengi wanakuwa kwenye majukumu ya timu za TAIFA. Kwa mfano kuna wachezaji wamefika jana na wengine wanaingia leo kwa mantiki hiyo lazima upate ugumu kwenye maandalizi lakini tutafanya kila liwezekanalo”

“Tunawaheshimu wapinzani wote tunaocheza nao ligi kuu. Ni kweli kesho tuna mechi ngumu kwani ni Derby, lakini tunajua namna tunauendea mchezo. Kila mara nasema mimi huwa sitazami sana historia. Yaliyopita yamepita, malengo yetu ni kutazama yanayokuja mbele yetu.” Miguel Gamondi