YANGA YASAHAU YALIYOPITA, KUINGIA KWA MPANGO KUIKABILI SIMBA
MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa amesahau matokeo yote yaliyopita hivyo kikubwa ni kusaka ushindi kwenye mchezo wa keso ambao ni Kariakoo Dabi, Uwanja wa Mkapa. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 kwenye Kariakoo Dabi, Yanga ilikomba pointi sita mazima ndani ya dakika 180 kwa kushinda nje ndani. Oktoba 19 2024 historia inakwenda kuandikwa…