>

RATIBA YA LIGI KUU BARA HII HAPA

BAADA ya Oktoba 2 2024 nyuki wa Tabora, Tabora United kupoteza mchezo wao wa ligi dhidi ya wakulima wa zabibu Dodoma Jiji kuna dakika 90 nyingine za kazi leo Oktoba 3 2024.

Ikumbukwe kwamba baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ulisoma Dodoma Jiji 2-0 Tabora United na mabao yalifungwa na Paul Peter dakika ya 46 na Wazir Junior alifunga bao la jioni dakika ya 90.

HII HAPA OKTOBA 3

KMC v Kagera Sugar, saa 10:00 jioni, Uwanja wa KMC Mwenge.

Yanga v Pamba Jiji, Uwanja wa AzamComplex saa 12:30 jioni.

Namungo v Azam FC saa 3:00 usiku, Uwanja wa Majaliwa.

Zote zitarushwa mubashara na Azam TV, burudani kwa wote.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, mtunzi wa kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371