OKOKA Mgavilenzi, Meneja Utekelezaji Sheria na kushughulikia malalamiko, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tazania, (TIRA) amesema kuwa wateja wanaopata matatizo kwenye soko la bima wanachotakiwa kufanya ni kufika kwenye mamlaka na watashughulikia haraka.
Mgavilenzi amesema kuwa wametoea elimu kwa Tanzania Insurance Brokers, (TIBA) kwa lengo la kuongeza ufanisi na weledi sokoni kwenye kutoa huduma kwa kuwa inawezekana.
“Wito wetu ni kwamba mteja anayepata tatizo kwenye soko la bima anachotakiwa kufanya ni kufika kwenye mamlaka ya bima, wale wote wanaotoa bima wamesajiliwa na kwa wale wanaokiuka sisi idara ya sheria tunahusika kushughulikia sheria na malalamiko kwa wakati.
“Wanaotoa huduma kwa njia za mtandao tumewasajili na huduma ambazo wanatoa ni halali na kama kuna changamoto ziwasilishwe kwenye mamlaka ya bima tutafanyia kazi kwa wakati.
“Tumewaeleza umuhimu wa kufanya biashara wakiwa wamesajiliwa na wakiwa walifanya usajili siku za nyuma wahakikishe wanahuisha usajili wao ili wapate uhalali wa kufanya biashara kwa kufuata sheria na kuzingatia sheria za bima kwa kufanya hivyo imani ya wananchi kwa kampuni za bima utaongezeka na ufanisi utaongezeka kwa kuwa wao wananafasi kubwa ya kuhakikisha tunapunguza malalamiko kwenye soko la bima.
“Kupata ufanisi kupata mafunzo na kuwa na soko salama lenye weledi, ushindani ambalo ni himilivu kuwasihi kushirikiana kwenye majukwaa mengine uwepo wa sheria mpya ya 2023 sheria ya bima kwa wote na kanuni zake zilizotoka 2024 wanapaswa kushiriki kwa kikamilifu na kutoa hamasa.”