USHINDI wa mabao 3-1 waliopata Simba mbele ya Al Ahli Tripoli unawapa tiketi ya kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika wakikomba milioni 15 za goli la mama.
Simba mabao yamefungwa na Kibu Dennis dakika ya 36 na bao la pili likafungwa na Leonel Ateba dakika ya 45.
Bao la tatu kwa Simba kwenye mchezo wa leo limefungwa jioni na kiungo mshambuliaji Edwin Balua ilikuwa dakika ya 89.
Rekodi zionyesha kuwa kipindi cha kwanza Simba ilipiga jumla ya mashuti manne yaliyolenga lango na katika hayo ni mawili yalifungwa huku wapinzani wao Al Ahli Tripoli wakipiga shuti moja lililolenga lango nalo likawa ni bao lililodumu mpaka mwisho wa mchezo.
Simba waliotea mara saba kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika na kiongozi aliyekutwa mara nyingi eneo hilo ni Ateba moja ni ileya dakika ya 63 ambayo alifunga bao likafutwa na mwamuzi wa kati.