>

KARIAKOO DABI INAFUKUTA HUKO NA MZIZIMA DABI

MSIMU wa 2024/25 ushindani wake unatarajiwa kuwa mkubwa kutokana na kila timu kujipanga kupata matokeo chanya kwenye mechi za ushindani ambapo kwa sasa ligi imesimama kwa muda kutokana na ratiba ya FIFA.

Wakati yote yakiendelea kuna fukuto ambalo lipo ikiwa ni kuelekea mechi kubwa Kariakoo Dabi na Mzizima Dabi ambazo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa wapinzani hao watakapokutana uwanjani.

Kwa upande wa Kariakoo Dabi inatarajiwa kuwa Oktoba 19 2024 Uwanja wa Mkapa ambapo awali ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Mwenge sasa itakuwa pale Uwanja wa Mkapa. Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imefanya maboresho katika ratiba kwenye mechi 14 ambazo zitakuwa na tarehe mpya hapo awali hazikuwa na tarehe.

Sababu kubwa ya maboresho hayo ni kuondolewa kwa klabu za Azam FC na Coastal Union katika anga la kimataifa kwenye hatua za awali. Azam FC ilifungashiwa virago na APR ya Rwanda kwa kufungwa jumla ya mabao 2-1 na benchi la ufundi lililokuwa chini ya Yusuph Dabo wamefungashiwa virago.

Mchezo wa mwisho kwa Dabo kukaa benchi ilikuwa kwenye ligi  alishuhudia ubao ukisoma JKT Tanzania 0-0 Azam FC huku Nado akiwa ni nyota wa kwanza msimu wa 2024/25 kupiga kona ndani ya kikosi cha Azam FC.

Katika maboresho ya ratiba, Mzizima Dabi ambayo itawakutanisha matajiri wa Dar, Azam FC v Simba inatarajiwa kuchezwa Septemba 26, Uwanja wa Mkapa.