MZEE WA WAA BADO ANA KIBARUA KIZITO SIMBA

STARAIKA refu kuliko goli ndani ya Simba, Steven Mukwala ana kibarua kizito ndani ya Simba kufunga mabao mengi ili kuongeza hali ya kujiamini kutokana na mwendo ambao ameanza nao kuwa wakusuasua katika kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Ikumbukwe kwamba nyota huyo haufunga kwenye mechi tatu mfululizo za ushindani ilikuwa Ngao ya Jamii hatua ya nusu fainali dhidi ya Yanga, Agosti 8 2024 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 0-1 Yanga na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Agosti 11 2024 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-0 Coastal Union.

Kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union alikosa nafasi ya dhahabu moja akiwa na mlinda mlango ambaye alikuwa shujaa kwenye pigo hilo baada ya kuokoa hatari.

Mchezo wa tatu ilikuwa dhidi ya Tabora United huu ulikuwa wa ligi ubao ulisoma Simba 3-0 Tabora United, Uwanja wa KMC, Mwenge Simba ilikomba pointi tatu mazima.

Bao lake la kwanza kwenye ligi amefunga mbele ya Fountain Gate ilikuwa ni Agosti 25 2024 Uwanja wa KMC, Complex alipokomba dakika 55.

Pongezi kwa Fikirini Bakari kipa wa Fountain Gate mzawa ambaye alitimiza majukumu yake licha ya kutunguliwa mabao manne.

Dakika ya 9, 16 na 21 Mukwala alikosa nafasi za wazi huku alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 43 wakati Simba ilipokomba pointi tatu.

Nyota huyo amesema kuwa ni furaha kwake kufunga ana amini watafanya vizuri kwenye mechi zinazofuata kutokana na ushirikiano ambao upo ndani ya timu.

“Tuna kazi kubwa ya kufanya kwa ajili ya kupata matokeo mazuri nina amini itakuwa hivyo na mazuri yanakuja mashabiki tuzidi kuwa pamoja.”