>

YANGA KWENYE KAZI KWA MARA NYINGINE TENA

BAADA ya kete ya kwanza kupoteza katika Mpumalanga Premier International Cup, Yanga inatarajiwa kuwa na kazi nyingine kusaka ushindi kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Jumatano ya Julai 24 Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhid ya TS GALAXY kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Mechi hii itapigwa kuanzia saa 10:00 jioni inatarajiwa kurushwa mubashara na Azam TV.

Julai 20 Yanga ilicheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa wa kirafiki baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-2 FC Augsburg.

Katika mchezo huo bao la kufutia machozi kwa Yanga lilifungwa na ingizo jipya ndani ya timu hiyo Jean Baleke aliyetumia pasi ya Maxi Nzengeli.

Ni dakika ya 85 ilikuwa Baleke alifunga bao kwa Yanga likiwa ni bao lake la kwanza akiwa na uzi wa Wananchi chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.