FEISAL SALUM YUPO HAPA KWA SASA, KAZI INAENDELEA

MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Yusuph Dabo Feisal Salum bado yupo ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2024/25.

Ilikuwa inatajwa kwamba Fei Toto alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba iliyokuwa inatajwa kwamba inahitaji saini yake.

Fei kwa wazawa ni namba moja kwenye kucheka na nyavu akifunga jumla ya mabao 19 huku kinara akiwa ni Aziz Ki wa Yanga aliyefunga jumla ya mabao 21.

Kwenye mazoezi ya Azam FC yanayondelea kwenye kambi ya Azam Complex nyota huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa kwenye kikosi hicho.

Dabo ameweka wazi kuwa mpango mkubwa ni kuwa bora kwenye mashindano ambayo wanashiriki ikiwa ni pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika na ligi.

“Tupo na mpango kazi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, tupo tayari kwa ajili ya kuwa bora ambapo tulianza na program ya GYM na nyingine zinafuata.”

Kambi ya Azam FC inatarajiwa kuwa sehemu tatu tofauti, Tanzania Bara na Visiwani na nje ya nchi pia wana mpango wa kuweka kambi huko.