MALIPO YA DUBE KUMALIZANA NA AZAM YAKWAMA NJIANI

Taarifa zilizo thibitika ni kwamba Prince Dube amelipa kiasi cha $200,000 kwenda kwa Azam fc ili kuwa huru.

Dube alifanya malipo hayo siku ya ijumaa jioni na kutuma vithibitisho vya malipo kwa uongozi wa Azam, uongozi wa Azam unakiri kupokea vithibitisho vya malipo hayo lakini mpaka sasa bado pesa hiyo haijafika kwenye akaunti ya Azam.

Dube alipaswa kulipa kiasi cha $300,000 kwa Azam ili kuwa huru, baada ya majidiliano ya pande zote mbili wakafikia makubaliano ya $200,000 na ndio yaliyo fanyika. Kwa mantiki hiyo Dube amelipa pesa yote inayo takiwa kulipwa.

Kinacho subiriwa sasa ni kiasi hiko cha pesa kuakisi kwenye akaunti ya Azam fc na kisha klabu kutoa tamko rasmi ya kumaliziana/kuachana na mchezaji huyo.