KIPA WA GUINEA AKAMATWA NA POLISI WA USWISI BAADA YA KUKUTWA NA COCAINE

Mlinda Mlango wa Guinea amekamatwa na Polisi wa Uswisi baada ya kukutwa na cocaine ikiwa ni baada ya kuhudhuria chakula cha jioni ambapo Aly Keita alidaiwa kunywa divai na baadaye dawa za kulevya.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea pia anashukiwa kwa utakatishaji fedha ya kiasi cha Euro 50,000

Aly Keita alikanusha taarifa hizo akitangaza kwamba alipata pesa hizo kutokana na timu ya taifa ya Guinea.

Klabu yake pia imemsimamisha kipa huyo wa Guinea hadi taarifa nyingine itakapotolewa.