SIMBA YAPITA NA MABAO 13 SHWAA

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika, Simba wamepita shwaa na mabao 13 mazima kwa msimu wa 2023/24 baada ya kuwapa mkono wa Thank You.

Timu hiyo imegotea nafasi ya tatu inaungana na Coastal Union ya Tanga kwenye Kombe la Shirikisho Afrika huku Yanga na Azam FC hizi zikiwa na kazi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwenye mpango kazi wa kuwaaga wachezaji wawili waliopewa Thank You walikuwa wakali wa kucheka na nyavu ikiwa ni nahodha John Bocco na Saido Ntibanzokiza.

Wawili hawa walihusika kwenye mabao 13 kwa kufunga ndani ya ligi ambapo ni mabao 59 timu hiyo ilifunga ikiwa namba tatu kwa safu ya ushambuliaji iliyofunga mabao mengi na iliongoza ni Yanga baada ya kufunga mabao 71.

Bocco hakuwa chaguo la kwanza kwenye mechi za ligi aligotea kucheza tano alifunga mabao mawili pekee huku Ntibanzokiza akifunga mabao 11 na alikuwa kinara kwa watupiaji ndani ya Simba.

Wote hawa wawili ni huru kwa sasa baada ya kupewa Thank You. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 Ntibanzokiza alitwaa tuzo ya ufungaji bora alifunga mabao 17 na alikuwa kwenye kikosi bora cha msimu lakini msimu huu ngoma ilikuwa nzito.