CHILUNDA NDO BASI TENA SIMBA

NYOTA wa Simba kwa msimu wa 2023/24 ambaye alikuwa ingizo jipya kwenye kikosi hicho ndo basi tena kwa msimu wa 2024/25 hatakuwa kwenye uzi wa nyekundu nyeupe.

Ni  Shaban Chilunda amekutana na Thank You kutoka kwa timu hiyo ambayo ipo kwenye maboresho kuelekea msimu mpya baada ya kugotea nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 69 tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya Azam FC iliyomaliza nafasi ya pili.

Taarifa kutoka Simba zimeeleza kuwa : “Shaban Chilunda hatakuwa sehemu ya timu yetu ya msimu ujao. Chilunda alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja weye kipengele cha kuongeza mkataba mwingine ikiwa atafanya vizuri. Alitolewa kwa mkopo ndani ya KMC hivyo mkataba wake umeisha rasmi.”

Anakuwa mchezaji wa tatu kupewa Thank You ndani ya Simba, alianza nahodha John Bocco Juni 17, Juni 18 ilikuwa ni zamu ya Saido Ntibanzokiza na Juni 19 ni zamu ya Chilunda.