HUYU MSHAMBULIAJI WA KAZI KWENYE RADA ZA SIMBA

WAKATI maboresho ndani ya kikosi cha Simba yakiendelea inatajwa kwamba kuna hesabu za kuinasa saini ya mshambuliaji wa KMC, Wazir Junior ambaye ni kinara kwa wakali wakutupia eneo la ushambuliaji.

Ikumbukwe kwamba Wazir ndani ya KMC ni mabao 12 alitupia na katika hayo mawili aliwafunga Simba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex langoni alianza mwamba Ayoub Lakred.

Inatajwa kuwa Simba inahitaji kupata mshambuliaji wa kazi ambaye atakuwa mzawa akishirikiana na wengine ambao watakuja kwenye dirisha la usajili ambalo lilifunguliwa Juni 15 2024.

Juni 17 mchezaji wa kwanza kupewa Thank You Simba alikuwa ni nahodha John Bocco ambaye ni mshambuliaji hivyo kwenye eneo la ushambuliaji nafasi yae inasaka mtu.

Simba msimu huu wamekuwa na changamoto katika eneo la ushambuliaji baada ya kuondoka kwa Jean Baleke na Moses Phiri jambo ambalo uongozi unatafuta washambuliaji wapya mapema.

Michel Fred na Pa Jobe hawajawa kwenye ubora jambo ambalo linaongeza nguvu kwa mabosi wa Simba kuwa bize kutafuta mshambuliaji asilia kwenye eneo hilo ili kuwa bora msimu ujao.