ISHU YA WACHEZAJI KUWA NA UMRI MKUBWA SIMBA YAFUNGUKA

WAKATI wakitajwa kuwa wachezaji wengi wa Simba miaka imekwenda jambo lililofanya wakashindwa kufanya vizuri ndani ya ligi na Ligi ya Mabingwa Afrika benchi la ufundi la Simba limefafanua kuhusu ishu hiyo.

Miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri ndani ya Simba ni pamoja na Saido Ntibanzokiza ambaye ni namba moja kwa utupiaji katika kikosi cha Simba akifunga mabao 11.

Simba imegotea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ambapo itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa na pointi 69 baada ya kucheza mechi 30 ambazo ni dakika 2,700.

Mgunda amesema kuwa suala la wachezaji kutajwa kuwa na umri mkubwa halina uhusiano na matokeo uwanjani kwa kuwa kila mmoja anafanya kazi yake kwa mujibu wa maelekezo ambayo yanatolewa na benchi la ufundi.

“Kuhusu umri kutajwa kuwa sababu hilo haliwezi kuwa kweli kwa kuwa kila mchezaji anacheza kwa mujibu wa maelekezo ya benchi la ufundi hivyo kinachotokea ni kile kinachofanyika uwanja wa mazoezi.

“Wachezaji wapo vizuri na wanafanya kazi kubwa kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja tuna amini kwamba itakuwa hivyo, mashabiki wazidi kuwapamoja nasi tutakuwa imara.”