BREAKING: JOHN BOCCO AKUTANA NA THANK YOU

MOJA ya washambuliaji bora ndani ya Bongo kwa wazawa ambaye alikuwa ndani ya kikosi cha Simba John Bocco amepewa mkono wa asante.

Nyota huyo kafunga zaidi ya mabao 100 ndani ya ligi akiwa ni mshambuliaji mwenye mabao mengi kwa wazawa rekodi ambayo inaishi.

Ipo wazi kwamba kwa msimu wa 2023/24 haukuwa bora kwake Bocco ambapo awali taarifa zilikuwa zinaeleza kuwa alipata maumivu kwenye maandalizi ya Mapinduzi 2024.

Alikuwa akikinoa kikosi cha timu ya Vijana Simba kwa kuwa ni kocha hivyo katika mechi za mzunguko wa pili hakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda.

Taarifa rasmi kutoka Simba imeeleza namna hii: “Nahodha wetu na mshambuliaji kinara John Bocco hatokuwa sehemu ya kikosi.”