DIARRA AZUA JAMBO JIPYA HUKO YANGA ISHU YA MKATABA

KIPA chaguo la kwanza ndani ya Yanga, Djigui Diarra anatajwa kuwa ameomba kuongezewa mshahara ili aendelee kutimiza majukumu yake ndani ya timu hiyo.

Ipo wazi kuwa Diarra ni moja ya makipa ambao wameleta ushindani mkubwa kwenye eneo la walinda mlango ambapo awali Aishi Manula wa Simba alijenga ufalme wake kwenye eneo hilo.

Taarifa zinaeleza kuwa kipa huyo ambaye ana uhakika wa namba kikosi cha timu ya taifa ya Mali, alijiunga na Yanga Agosti 8, 2021 akitokea Stade Malien ya nchini kwao, amewaambia mabosi wa Yanga kuwa thamani yake imepanda zaidi.

Kutokana na thamani ya ligi kupanda pia anahitaji kuona kwamba hadi kwenye upande wa maslahi yanafanyiwa kazi kwa kuboreshewa masilahi.

.
Mkataba wake ndani ya Yanga unagota mwisho Januari 2025 baada ya kuongeza kandarasi mpya msimu uliopita kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Ipo wazi kuwa msimu wa 2023/24 Yanga imetwaa taji la ligi ikiwa ni mara tatu mfululizo wakifanikisha mpango kazi huo na pia walifunga msimu kwa kutwaa CRDB Federation Cup mbele ya Azam FC.