JEMBE AZUNGUMZIA MKATABA WA JOBE NA MANGUNGU KUSAJILI

LEGEND kwenye masuala ya uandishi wa Habari Bongo, Saleh Jembe ameweka wazi kuwa ikiwa Mangungu ataachiwa suala la usajili inaweza kuwa ni mzigo mzito zaidi kwake akibainisha kwamba kwa sasa Simba wanahitaji marekebisho ya timu yao na wapunguze maneno mengi zaidi wafanye kazi kwa ushirikiano zaidi. Ameweka wazi kuwa kati ya timu ambayo imeongoza kwa kufanya makosa mengi kwenye usajili ni Simba.