USHINDI WA TAIFA STARS, WAZIR AFICHUA SIRI

WAZIR Junior mfungaji wa bao pekee la ushindi kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Zambia ameweka wazi kuwa ushirikiano kutoka kwa wachezaji wengine uliwapa nguvu ya ushindi katika mchezo huo.

Tanzania ipo kundi E ambapo vinara ni Morocco wenye pointi 6 baada ya kucheza mechi mbili huku Tanzania ikiwa nafasi ya pili na pointi 6 baada ya kucheza mechi tatu.

Niger nafasi ya tatu, Zambia nafasi ya nne zina pointi tatu huku Congo nafasi ya tano na Ertrea nafasi ya sita hazijakusanya pointi.

Junior ambaye alifunga bao dakika ya 5 amesema walikuwa wakipewa maelekezo kutoka kwa wachezaji wenye uzoefu na kuonyesha ushirikiano mwanzo mwisho.

“Ulikuwa ni mchezo wenye ushindani na kila mchezaji alikuwa akipambana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri. Maneno kutoka kwa wachezaji wenye uzoefu ikiwa ni Himid Mao, Mohamed Hussein yalikuwa yanatupa nguvu kwenye mapambano na mwisho tukapata ushindi kwenye mchezo wetu.”