Klabu ya Feyenoord ya Uholanzi imemteua mkufunzi Brian Priske kuwa kocha mkuu klabuni hapo akichukua mikoba ya Arne Slot aliyetimkia Liverpool.
Priske (47) raia wa Denmark ambaye amewahi kuinoa klabu ya Royal Antwerp ya Ubelgiji hivi karibuni alikuwa akiifundisha klabu ya Sparta Praha ambayo ameiongoza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Jamhuri ya Czech mara mbili mfululizo.