>

BREAKING: MWENYEKITI WA BODI SIMBA AJIUZULU, AMTANGAZA MO DEWJI KURUDI

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya klabu ya Simba Sc Salim Abdallah “Try Again”  ametangaza kujiuzulu kutoka kwenye nafasi hiyo kwenye mazungumzo yake jioni leo Juni 11, 2024  kupitia Insta Live kwenye ukurasa rasmi wa Simba SC amesema, Mohammed Dewji atarudi kuwa mwenyekiti wa Bodi kama awali.

“Kwa maslahi mapana ya Simba kwa kutambua mpira ni mchezo wa hisia, Mimi kama Mwenyekiti wa Bodi nimemwomba Mwekezaji wetu Mohamed Dewji MO arejee kama Mwenyekiti wa Bodi nami nitasalia kama Mwanachama na Kiongozi ambaye nipo tayari wakati wowote kuitumikia Simba, kwa maana hiyo natangaza kuondoka kwenye kiti”- Salim Abdallah Try Again, Mwenyekiti wa Bodi ya Simba kupitia