SIMBA YAKAMATIA REKODI HII BONGO

LICHA ya kugotea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na kusepa na tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika ikiungana na Coastal Union ya Tanga.

Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu Juma Mgunda ambaye funga kazi yake ilikuwa Mei 28 Uwanja wa Mkapa aliposhuhudia ubao ukisoma Simba 2-0 JKT Tanzania mabao yakifungwa na Saido Ntibanzokiza na Willy Onana.

Simba inaingia kwenye timu yenye rekodi ya kuwa timu ambayo imefunga bao kwenye kila mchezo ndani ya ligi msimu wa 2023/24 licha ya kugotea ikiwa nafasi ya tatu.

Katika mechi 30 ambazo ilicheza timu hiyo safu yake ya ushambuliaji ilifunga jumla ya mabao 59 ikiwa ni namba tatu pia kwa timu ambazo zimefunga mabao mengi kwenye ligi.

Namba moja ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambayo ilimaliza msimu ikiwa na mabao 71 kinara wa utupiaji akiwa ni Aziz KI aliyefunga jumla ya mabao 21 ndani ya ligi.

Ki ni mkali wa mguu wa kushoto ambapo alitumia mguu huo kufunga mabao 17 na mabao matatu alifunga kwa kutumia mguu wa kulia na bao moja alifunga kwa pigo la kichwa ilikuwa dhidi ya Tabora United mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.