YANGA WANA JAMBO LAO KUBWA

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga wana jambo lao kubwa Juni 9 2024 ambapo ni Mkutano Mkuu wa Wanachama, (Annual General Meeting-AGM).

Ni wazi kwamba chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi Yanga imetwaa taji la Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 80 na ilitwaa taji la CRDB Federation Cup kwa ushindi dhidi ya Azam FC kwenye fainali iliyochezwa Juni 2 2024.

Ilikuwa ni Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar, dakika 120 ngoma ilikuwa Azam FC 0-0 Yanga na kwenye changamoto ya penalti ilikuwa Azam FC 5-6 Yanga langoni alikuwa ni Djigui Diarra kwa Yanga na Azam FC ni Mustapha Mohamed.

Kamati ya Utendaji ya Yanga chini ya Rais Hersi Said leo Juni 2024 ilifanya kikao maalumu kwa ajili ya maandalizi ya AGM)kilichofanyika katika ukumbi wa Urban By City Blue, Masaki Jijini Dar.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Posta, Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo hata ule uliopita 2023 ulifanyika hapo kwa wanachama waliokidhi vigezo kuhudhuria mkutano huo.

Taarifa rasmi kutoka Yanga imetaja baadhi ya matawi ambayo yamekidhi vigezo vya kushiriki yakiwa yameongezeka ikiwa ni pamoja na GSM Family, Yanga B.O.T, Yanga Alliance, Brotherhood VIP na Magomeni Makuti yote ya Dar.