YANGA YAFICHUA SIRI YA UBINGWA CRDB FEDERATION CUP

MIGUEL Gamondi Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa ukomavu wa wachezaji wake kwa kukubali matokeo kwenye mchezo huo yaliwapa nguvu ya kuendelea kupambana mpaka mwisho wa mchezo.

Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa wa CRDB Federation Cup wakipeta mbele ya Azam FC matajiri wa Dar ambao walikuwa kwenye nafasi nzuri ya kutwaa taji hilo bahati haikuwa yao.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, dakika 90 ziligota mwisho ubao ukisoma Azam FC 0-0 Yanga na dakika 30 nazo ngoma ilikuwa vilevile kwa timu zote hivyo ndani ya dakika 120 ngoma ilikuwa nzito kwa kuwa nyavu hazikutikisika.

Gamondi amesema kuwa: “Kwenye penalti baada ya wachezaji wawili kukosa, bado tulikuwa na imani kwamba haijaisha mpaka iishe na mwisho tumefanikisha malengo tukitwaa ubingwa hii ni furaha kwetu.”

Azam FC walipata penalti 5-6 Yanga ambao ni mabingwa wapya wa CRDB Federation Cup msimu wa 2023/24.

Kwenye penalti Yanga walianza kukosa kupitia kwa Aziz KI na mpigaji wa pili pia ambaye ni Joseph Guede alikosa baada ya mikono ya Mustapha Mohamed kufanya kazi yake huku wapigaji wawili wa mwanzo kwa Azam FC wakifunga ni Adolf Mutasiga na Sidibe na mpigaji wa tatu kwa Azam FC ambaye alikuwa wa kwanza kukosa alikuwa ni Yusuph Foutens.

Azam FC walishinda jumla ya penalti 5-6 Yanga wakitwaa taji la nne wakiwa ni namba moja kwa timu iliyotwaa mataji mengi ya CRDB Federation Cup ambapo awali ilikuwa inaitwa Azam Sports Federation kwa sasa ina wadhamini wapya na timu ya kwanza kutwaa taji hilo ni Yanga.